MWANAMKE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTELEKEZWA NA MUMEWE,WANAWAKE WALAANI



Wanawake wa Mtaa wa Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wamelaani vikali kitendo cha Abdalla Ibrahim Mkazi wa mtaa huo kumtelekeza mkewe Rosemary Robert Ismail mpaka kusababisha kifo chake kwa kutompatia huduma baada ya kuugua kwa muad mrefu.
Wanawake hao wamesema kitendo ambacho amekifanya Bw.Ibrahimu ambaye ni mlinzi wa kampuni moja mjini Mpanda ni ukatiri wa hali ya juu.
Kwa upande wake Muuguzi wa wagonjwa Majumbani Hadija Mwishehe mkazi wa mtaa wa Mpanda Hotel amesema, alimpatia huduma ya kwanza mwanamke huyo akiwa nyumbani kabla ya kufariki juzi akiwa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa matibabu zaidi.
Hata hivyo Bw.Abdalla Ibrahim ambaye ni mume wa Rosemary Robert Ismail amekana kumtelekeza na kumnyima huduma huku akisema kuwa ameishi naye kwa muda wa wiki moja.
Kwa mjibu wa Bw.Benson Soyi ambaye ni jamaa wa karibu na marehemu,mpaka sasa ndugu wanaosemekana kuwa wapo Sumbawanga Rukwa hawajapatikana na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Naye Tekra Pius Kabedi ambaye ni Mjumbe wa serikali ya Mtaa Mpanda Hotel amethibitisha kupokea taarifa za kifo hicho mtaani kwake ambapo amesema sababu kubwa ni kukosa kupewa huduma ya matibabu na chakula.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA