SERIKALI YAKANUSHA SUKARI YA ZANZIBAR KUZUIWA KUUZWATANZANIA BARA


Serikali imekanusha taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba imekizuia Kiwanda cha Sukari Zanzibar,ZSFL kuuza Sukari yake Tanzania Bara.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas
Akizungumza jana jijini Arusha,Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas amesema, kiwanda hicho kinapaswa kukidhi soko la Zanzibar la tani elfu 10 badala ya kulalamika kimezuiwa kuuza Sukari nje.
Dk.Abbas amesema mahitaji ya kawaida Zanzibar ya sukari ni Tani elfu 17 mpaka elfu 20 kwa mwaka lakini kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani elfu 10 japo kwa sasa uzalishaji umeshuka hadi tani elfu 8 hivyo kufanya Zanzibar kuwa na upungufu wa tani elfu 9 hadi elfu 12.
Mapema wiki hii,Kaimu Mkurugenzi Mkuu Kiwanda hicho cha Sukari Zanzibar,Bi. Fatma Salum Ali,alisema kiwanda hicho kinapata hasara ya zaidi ya shilingi laki tatu kwa kila tani moja ya Sukari inayozalishwa kutokana na kushindwa kupata kibali cha kuuza Sukari Tanzania Bara ambako kuna soko shindani kwa misingi ya gharama za uzalishaji na bei.
Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA