MWANASHERIA MKUU WA KENYA PROFESA GITHU MUIGAI ABWAGA MANYANGA


Mwanasheria mkuu wa Kenya Profesa Githu Muigai amejiuzulu baada ya kuhudumu kwa miaka sita na nusu ambapo kufuatia uamuzi huo Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa huduma zake na sasa jaji Paul Kihara Kariuki atachukua mahala pake.
Kabla ya uteuzi wake kuwa mwanasheria mkuu profesa Muigai alikuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni ya mawakili ya Mohammed Muigai na amekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi.
Mwanasheria mkuu wa Kenya Professa Githu Muigai
Haki miliki ya picha
Mwanasheria mkuu wa Kenya Professa Githu Muigai
Aidha alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha sheria cha Columbia mjini New York ambapo Kutoka 1984 alikuwa mwanfunzi katika chuo cha kusomea uanasheria nchini Kenya .
Wakati huo huo alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi huku akiwa mshauri wa serikali katika maswala ya kisheria, Githu Muiga atakumbukwa kwa kuleta sheria za mageuzi katika timu ya uchaguzi nchini Kenya siku chache tu kabla ya uchaguzi kufanyika.
Katika sheria hiyo kamishna yeyote yule katika tume ya uchaguzi alipewa nguvu za kumtangaza mshindi wa uchaguzi iwapo mwenyekiti wa tume hiyo hayupo.
Sheria hiyo ilizua pingamizi kutoka kwa upinzani pamoja na jamii ya kitaifa waliodai kuwa serikali haiwezi kufanya mabadiliko ya sheria za uchaguzi wakati ambapo uchaguzi mkuu unakaribia.
Katika hatua nyingine Githu Muigai atakumbukwa katika  hatua ya kuliharamisha kundi la upinzani la NRM hatua ambayo pia ilipingwa na viongozi wa upinzani wakisema kuwa ni hatua mojawapo ya serikali ya kutaka kukandamiza upinzani.
Siku chache kabla ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyejiita kuwa 'rais wa wananchi' kula kiapo,Bwana Githu alitishia kuwa mtu atakayejaribu kula kipao cha urais atajilaumu mwenyewe kwa kuwa mashtaka yatakayomkabili ni ya uhaini ambao hukumu yake ni mtu kunyongwa.
Hatahivyo Raila alikula kiapo hicho katika bustani ya Uhuru Park katika hafla iliohudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa upinzani na matokeo yake yalisababisha viongozi wa karibu walioshiriki katika kumlisha bwana Raila Kiapo hicho kukamatwa na kushatkiwa huku wengine wakifurushwa kutoka nchini.
Hatahivyo viongozi wengine wakuu wa upinzani hawakuhudhuria hafla hiyo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA