DR. SHEIN AAGIZA WIZARA YA ELIMU KULIPA MADENI YOTE YA WALIMU KABLA 2019



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein amesema sera ya elimu bure  kwa wanafunzi wa sekondari itaanza ifikapo  mwezi june  mwaka huu.
Akizungumza  katika Mkutano Mkuu wa Sita wa chama cha walimu Zanzibar zatu amesema serikali imeamua  kuondoa ada  kwa wanafunzi  kwa lengo la kuendeleza sera ya rais wa awamu ya kwanza Shekh Abeid Amani Karume.
Amesema  sera ya elimu bure itaimarika endapo walimu watafanya kazi kwa mujibu wa sheria na maendeleo ya elimu yatajengeka iwapo  walimu watakuwa na juhudi  na uimara pamoja na misingi  bora na zamira njema ya kufundisha wanafunzi maskulini.
Dr.shein amesema anatambua matatizo yanayowakabili walimu  pamoja na skuli kukabiliwa na matatizo mbalimbali  yakiwemo uhaba wa walimu, uchache wa vifaa vya kufundishia pamoja na malimbikizo ya madeni ya mishahara ya walimu na kuiagiza wizara ya elimu kuhakikisha wanawalipa  madeni yote  wanayodaiwa na walimu  kabla ya kufikia 2019 kwani kuendelea deni hilo litaweza kuondoa ari ya walimu kufundisha na kupelekea sekta ya elimu kuyumba kutokana na maslahi madogo ya walimu.
Hata hivyo  Rais Shein amesema amerizishwa na matokeo yaliyopatikana katika mitihani ya taifa  kwa elimu ya msingi na sekondari na kuitaka wizara ya elimu  kukaa pamoja na skuli zote za Zanzibar zile  zilizofanya vibaya katika mitihani ya taifa ili kuweza kujua  sababu  zilizopelekea kufeli.
Aidha amesema serikali itaendelea kujali na kuthamini michango ya walimu  yanayotoka katika taifa  kwa kujali maslahi yao kila uchumi wan chi utakavyo imarika.
Kwaupande wake Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar zatu Mussa Omar Tafurwa Mapema akisoma risala ya walimu amesema miongoni mwa matatizo yanayowakabili ni tatizo la uhaba wa walimu kwa skuli za pemba  na mikoa ya kaskazini  na kusini  kwa unguja.
Tafurwa ameiyomba serikali  kufanya uwekezaji wa  rasilimali   fedha ya kutosha ili kuweza kuajiri walimu pamoja,kununulia vifaa vya kufundishia pamoja na  kulipa madeni ya walimu wanayodai kwani pia baadhi yao wamesha staafu na wengine kufariki.
Amesema pia licha ya matatizo hayo pia  walimu wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufundishia ambapo hupelekea kuumwa na kushindwa kufanya kazi vizuri  hivyo wameiyomba serikali  kuwaanzishia bima ya afya  kwani wanashindwa mukumu gharama za matibabu  kwani fedha wanayoipata  bado haikidhi haja.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
                                                                                            

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA