ACT- WAZALENDO KUZUNGUKA MIKOA 5 UKIWEMO KATAVI
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo
Ndugu Dorothy Semu,anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mikoa mitano ya
Tanzania Bara akiambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Aidha taarifa ya Chama hicho
imebainisha kuwa katibu ataambatana na Ndg.Wilson Mshumbusi ambaye ni Mwenyekiti
wa Ngome ya Wazee Taifa,Ndg.Janeth Rithe ambaye ni Katibu wa Bunge na Serikali
za Mitaa pamoja na Katibu wa Sera na Utafiti Ndg.Idrisa Kweweta.
Moja ya majukumu ambayo Dorothy Semu
atayafanya ni kukagua uhai wa Chama,kutoa maelekezo ya ujenzi wa chama,
kusikiliza Kero na changamoto za wanachama na kuzipatia ufumbuzi.
Mbali na hayo Katibu Mkuu huyo pia
atakagua maendeleo ya zoezi la uchaguzi wa ndani ya chama huku ikielezwa kuwa
ziara hiyo pia itawalenga wanachama na viongozi wa ACT Wazalendo wa maeneo
hayo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments