WAKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO WAMELALAMIKA KUNYANG’ANYWA GARI LA WAGONJWA,HALMASHAURI YATOA UFAFANUZI

Na.Issack Gerald
Wakazi wa kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa madai kuwa halmashauri hiyo imewanyanga’anya gari la wagonjwa ambalo limekuwa likitoa huduma kwa wagonjwa katika kata hiyo.
Wamesema kuwa wamenyang’anywa gari kwa madai kuwa wakazi wa Katumba hawana dereva wa kuendesha gari hilo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mh.Raphael Kalinga amekanusaha kuwanyang’anya gari la wagonjwa wakazi wa Kata ya Katumba ambapo amesema lipo kwenye matengenezo baada ya kuharibika.
Aidha Kalinga amesema suala la kuharibika kwa gari hilo limekwishatolewa ufafanuzi kuanzia kwa viongozi wa Halmashauri,Mkoa hadi ngazi ya wizara.
Kata ya Katumba ina vijiji 16 na zaidi ya wakazi elfu hamsini wanaotegemea huduma ya gari hilo.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA