MENEJA MPANDA RADIO FM ATOA NENO KWA WANASALAAM,LEO KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI


Na.Issack Gerald
Wadau wa salaamu kupitia vyombo vya habari Mkoani Katavi,wameaswa kushiriki kwa kiasi kikubwa kuibua masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuibua matukio yanayoiathiri jamii kama ukatiri.
Baadhi ya watuma Salaamu Mkoani Katavi wakiwa katika kikao na watumishi Mpanda Radio katika Ukumbi wa Mpanda Radio(PICHA NA.Issack Gerald)
Wito huo umetolewa leo na Meneja wa kituo cha Mpanda Radio Bw. Revocatus Msafiri,wakati akizungumza na viongozi wa vikundi vya wanasalaamu kuanzia ngazi ya kata hadi Mkoa kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa studio ya Mpanda Radio.
Katika hatua nyingine, Bw.Msafiri amesema bonanza la leo la mchezo wa mpira wa miguu baina ya watumishi Mpanda Radio na watuma salaamu Mkoani Katavi linalenga kupanua wigo wa kufahamiana na kuongeza mahusiano yenye tija  kwa jamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mpanda Radio
Kwa upande wao watuma salaamu mbali na kuipongeza Mpanda Radio kwa matangazo yanayozingatia  mahitaji ya jamii,pia wamekiomba chombo hiki cha habari kuwafikia zaidi wananchi waishio vijijini kutokana na vyombo vya habari kutofika mara kwa mara.

Kituo cha Mpanda Radio ambacho ni cha Kijamii kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2013 kikiwa na lengo la kuelimisha,kuhabarisha na kuburudisha jamii na kilizinduliwa na mwenge wa uhuru Julai 17 mwaka 2017.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA