UTATA WAIBUKA UGAWAJI VIWANJA WAHANGA WA BOMOABOMOA MKOANI KATAVI

Na.Issack Gerald-Katavi
WAKAZI wa Mitaa ya Msasani na Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameeleza kutoridhishwa na mwenendo wa ugawaji viwanja katika mtaa wa kampuni kata ya Misunkumilo wanakotakiwa kuhamia.

Wakizungumza kwa masikitiko ya kutoelewa hatima ya wanakotakiwa kujenga makazi yao wamesema,wamesikitishwa na kauli ya Mstahiki Meya Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo kwamba wanaotakiwa kupewa viwanja kwa sasa ni wazee, wajane  na wasiojiweza huku wengine wakiachwa bila kujua hatima yao kwa sasa.
Miongoni mwa wakazi wa msasani na Tambukareli ambao wamezungumzia utata wa ugawaji viwanja ni pamoja na Joyce Kledo Myomba,Tito Emmanuel,Magiroya Mkautani,Juliana Paul Mgawe,Aurelia ambapo pia wamedai kuwa ikiwa watapelekwa wazee na watu wasiojiweza katika eneo hilo pekee yao ni kudumaza maendeleo suala ambalo limeungwa mkono na baadhi ya wazee wakisema inatakiwa iwe mchanganyiko ili washiriki kwa pamoja kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Willium Mbogo amekanusha eneo la kampuni kupewa wazee,wajane na wagonjwa peke yao ambapo amesema mgao huo utafanyika kwa wahanga wote isipokuwa kipaumbele kimetolewa kwa wasiokuwa na uwezo wakiwemo wazee.
Aidha amesema mgao huo wa viwanja unaofanyika kwa kuzingatia agizo la mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi ambaye ndiye aliyenunua viwanja kwa ajili ya wananchi hao,ni ugawaji wa viwanja bure
Wakati huo huo Serikali za mitaa ya Msasani na Tambukareli wameagizwa kufanya mikutano ya hadhara kuanzia kesho ili kuwashirikisha wananchi juu wa wananchi wa awamu ya kwanza wanaotakiwa kupewa viwanja ambapo kila mtaa umepewa viwanja 75.
Sakata la baadhi ya wakazi kutakiwa kuondoka katika eneo ya hifadhi ya reli lilianza kuibuka mwezi juni mwaka huu ambapo kutokana na ukosefu wa maeneo wanakotakiwa kujenga makazi mapya ili kupisha eneo la reli kulisababisha wakazi hao kuongezewa miezi 6 na kutakiwa kuondoka kabla ya mwezi Januari kupisha bomoa bomoa.
Kaya zaidi ya 200 za mitaa ya Msasani na Tambukareli zinatakiwa kuondoka baada ya kuathiriwa na agizo la Shirika la reli Tanzania TRL.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA