WAKAZI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI WATAKIWA KURIPOTI UKATIRI WA KIJNSIA-Septemba 18,2017



WANANCHI wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kufichua matukio ya ukatiri wa kijinsia yanayofanyika na kupelekea madhara kwa wanaotendewa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkaguzi wa Polisi Wilayani Mpanda ambaye pia ni kaimu mkuu wa Kituo cha Polisi Insepcta Stephen Kisaka ambapo amesema makundi ya watoto na wanawake yanaathirika kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Afisa wa dawati na jinsia na watoto Wilayani Mpanda ambaye pia ni Polisi Kata Kata ya Makanyagio Inspecta Mwanaisha Lwano,wamawataka wananchi kutoa taarifa za ukatiri kwa watoto,wanawake na makundi mengine ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Kwa upande wao wananchi wameahidi kutoa ushirikiano ili kutokomeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa inayotajwa kuwa na ukatiri kwa kiwango kikubwa ambapo miongoni mwa chanzo ni mfumo kandamizi kwa baadhi ya familia.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA