WAKAZI KATAVI WALALAMIKIA KUKITHIRI KWA TAKA KATIKA MAKAZI YAO-Septemba 21,2017



WAKAZI wa kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wamelalamikia uwepo wa taka katika makazi yao kwa muda mrefu hali inayosababisha kuhofia magonjwa ya mlipuko.

Wamesema uchafu umerundikana majumbani na barabarani kwa Zaidi ya wiki tatu bila kuzolewa licha ya kila mwezi kuchanga pesa kwa ajili ya uzoaji taka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha kuzoa taka katika Kata ya Mpanda Hotel Bw. Emmanuel Mgiuna amesema wanashindwa kuzoa taka kwa sababu hakuna gari wala kizimba kwa ajili ya kukusanyia uchafu.
Afisa mtendaji wa kata ya Mpanda Hotel Bw.Hamidu Sungura amekataa kuzungumzia tatizo la mrundikano wa taka katika maeneo mbalimbali ya Kata ya Mpanda Hotel kwa muda mrefu huku naye Bibi Afya wa kata hiyo Bi.Grace Kunchela kwa sharti la kutorekodiwa sauti akisema zoezi la kuzoa litaanza kesho.
Tatizo la kukithiri kwa taka katika maeneo mbalimbali katika manispaa ya Mpanda kumetokea kutokana na kutokuwepo kwa magari ya kutosha kwa ajili ya kauzoa taka pamoja na vizimba vya kukusanyia taka.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com,Ukuasa wa Facebook P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA