KIWANDA CHAKOSA CHOO,WANANCHI WAKERWA NA HARUFU MBAYA,MWENYE KIWANDA ARONGA-Septemba 21,2017



Kiwanda cha kupasulia magogo kilichopo kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi chenye zaidi ya wafanyakazi 20 hakina huduma ya choo.

Wakizi wa eneo hilo ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema wanakabiliwa na harufu mbaya kwa muda mrefu kutokana watu kujisaidia hovyo katika maeneo hayo hasa shughuli zinapoendelea kufanyika katika kiwanda hicho.
Mmiliki wa kiwanda hicho ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Bilali amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuahidi kulipatia ufumbuzi ndani ya muda mfupi.
Aidha ameongeza kusema kuwa kiwanda hicho kilisimama uzalishaji kutokana na serikali kusitisha uvunaji wa bidhaa za misitu hivyo kuathiri shughuli za uendelezaji wa kiwanda hicho
Serikali kupitia mmalaka zake imekuwa ikisisitiza ujenzi wa vyoo bora katika maeneo ya makazi na taasisi mbalimbali ili kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com,Ukurasa wa Facebook-P5Tanzania Limted

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA