WAKAZI KATA YA MPANDA HOTEL WAELEZEA KUFURAHISHWA NA HATUA YA KUTATUA TATIZO LA MAJI-Septemba 29,2017

Na.Issack Gerald-Katavi
BAADHI ya wakazi wa kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wameelezea kufurahishwa na hatua ya uchimbaji mitaro ya kupitisha mabomba kwa ajili ya kuleta huduma ya maji katika katika kata hiyo.

Wakazi hao wakiwemo Anna Fabian Katikisha na Omerina Vyakuziwa,wamesema ikiwa maji ya kutosha yataletwa kutaondoa tatizo la maji ambalo limekuwepo kwa zaidi ya miaka thelathini.
Aidha wakazi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitegemea maji kutoka kata jirani za Makanyagio, Misunkumilo, Mwangaza na Magereza.
Katika hatua nyingine wamesema kutokana na uhaba kwa maji muda mrefu katika kata hiyo,hata matumizi ya vyoo vya kisasa imekuwa changamoto kuvitumia kwa kuwa vinategemea maji.
Julai 22 mwaka huu,diwani wa kata ya Mpanda Hotel Willium Liwali alisema kata ya Mpanda Hotel imepata zaidi ya Shilingi milioni 21 ili kukabiliana na tatizo la maji ambalo limeikumba kata hiyo kwa muda mrefu.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

                                                       

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA