HALMASHAURI ZOTE MKOANI KATAVI ZATAKIWA KUANDAA VITAMBULISHO VYA WAZEE-Septemba 28,2017

Na.Issack Gerald-Katavi

Halmashauri  zote Mkoani Katavi zimetakiwa kuandaa vitambulisho kwa wazee wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa matibabu bure.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa mkoa wa katavi Dk. Yahaya Hussen wakati akizungumza na Mpanda Redio na kusema kuwa hatua hiyo itarahisisha utambulisho kwa wazee ambao hawana kadi za matibabu.
Dk Yahaya ametaja vigezo ambavyo mzee anapaswa kupatiwa matibabu bure kuwa ni kuanzia umri wa miaka 60 pamoja na uwezo wa maisha.
Kuhusu suala la mzee kupewa kipaumbele katika matibabu Dk. Yahaya amesema katika wilaya ya Mpanda ipo zahati kwa ajili ya matibabu kwa wazee sambamba na kuweka matangazo ya Mpishe mzee apate matibabu  katika zahanati na vituo vyote vya  Afya.
Kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,mkoa wa Katavi ulikuwa na wazee zaidi ya elfu tano(5000).
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited





Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA