WAISLAMU KATAVI WATAKIWA KUWA WAMOJA NA WENYE MOYO WA HURUMA-Septemba 1,2017

WAISLAMU mkoani Katavi wametakiwa kuwa wamoja na wenye mshikamano katika hali mbalimbali ya maisha ya kila siku wanayopitia bila kujali itikadi ya chama,rangi,dini,kabila wala taifa analotoka kwa kuwa wote ni binadamu ambao wameumba na mwenyezi mungu.


Wito huo umetolewa na Kaimu shehe mkuu wa Mkoa wa Katavi Shehe Nassoro Kakulukulu,katika swala ya baraza la Eid ambayo imeswaliwa katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.
Aidha Shehe Kakulukulu ambaye pia ni Mjumbe wa baraza la mashehe Mkoa na mjumbe wa Halmashauri kuu taifa amesema,waislamu wanatakiwa kuvumiliana kwa sababu mungu ameumba watu mbalimbali wenye fikra na akili tofauti.
Kwa upande wake Khershah Fazal ambaye ni Mwenyekiti wa mkoa wa Katavi wa taasisi ya Markaz Tabligh yenye makao makuu Kiwalani Jijini Dar es salaam amesema,waislamu wanatakiwa kupendana,kusaidiana na kuoneana huruma wao wenyewe wakati wa shida pamoja na kuzingatia amri za mwenyezi mungu kwa vitendo.
Sala ya baraza la Eid ya mwaka 1438 wa kiislamu ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wakiwemo katibu wa bakwata Wilaya ya Mpanda Shehe Omary Muna,wajumbe wa baraza kuu ngazi ya taifa,mashehe wa misikiti ngazi ya mitaa,wilaya na mkoa.
 Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA