VIBOKO MKOANI KATAVI WASABABISHA NDOA KUVUNJIKA PIA UHARIBIFU WA MAZAO SHAMBANI-Septemba 29,2017



Mfano wa picha ya viboko vinavyopatikana mto sitalike mkoani katavi
Na.Issack Gerald-Katavi
WAKAZI wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo katika Manispaa ya Mpanda,wameilalamikia serikali kutochukua hatua dhidi ya viboko waliopo bwawa la Milala vinavyoharibu mazao shambani na kutishia uhai wa binadamu mara kwa mara.

Wakazi hao wakiwemo Masoud Mawisa na Adam Said Kanyamaso kutoka mitaa ya Kigamboni,Misunkumilo na Makanyagio wamesema,madhara mengine ambayo yametokana na viboko hao ni kuvunjika kwa ndoa zao kutokana na wanaume kuhamishia makazi yao shambani ili kudhibiti
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Misunkumilo Bw.Antipas Kalumbete ambaye pia ndiye anayekaimu nafasi hiyo katika kijiji cha Milala,amethibitisha viboko hao kuwa tishio wa wakazi wa maeneo hayo akisema kuwa maliasili waliandikiwa barua lakini mpaka sasa hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa dhidi ya wanayama hao.
Bwawa la milala ambalo ni miongoni mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda inasemekana kwa sasa lina viboko zaidi ya tehelathini huku wakazi wa maeneo jirani na bwawa hilo wakilazimika kujifungia ndani majira ya jioni wakiogopa kushambuliwa.
Viboko hao wanadaiwa kutoka katika mto Katuma uliopo kata ya Sitalike palipo na shule kubwa ya viboko ambapo hata hivyo hakuna uhusiano wa sitalike na bwawa la milala kwa kuwa viboko hao wametoroka na kupitia nchi kavu ambapo umbali kutoka Bwawa la Milala mpaka Sitalike ni takribani kilomita 60.
Kumekuwa na matukio ya wanayama pori kutoroka katika hifadhi zao na kusababisha madhara kwa binadamu ambapo wanyama wengine ambao wamekuwa wakitoroka katika hifadhi na kuvamia makazi ya watu na kusababisha madhara kwa watu ni Simba.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA