TANROADs MKOANI KATAVI WATAJWA KUSABABISHA AJALI-Septemba 22,2017



Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
BAADHI ya wakazi wa wanispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameilalamikia Wakala wa barabara TANROADs Mkoani Katavi kwa kupuuzia uwekaji alama za usalama barabarani katika eneo la Super City mtaa wa Majengo eneo ambalo limekuwa likisababisha ajali mara kwa mara.

Wakizungumza na Mpanda Radio katika eneo hilo,wakazi hao wakiwemo Rajabu Ally Hussein na Ramadhan Fadhili wamesema kila wakati ajali hutokea katika eneo hilo kutokana na kutokuwepo matuta,mzunguko na alama nyingine zinaoonesha kuwepo kwa alama ya makutanio ya barabara.
Taarifa kuhusu matukio ya ajali yanayoendelea kutokea katika eneo la Super City Mtaa wa Majengo inafahamika kwa wakala wa Barabara TANROADs kwa sababu Wiki mbili zilizopita Mhandisi wa TANROADs Mkoani Katavi Frank Mwakisonga alidai aandikiwe barua ndipo azungumze na chombo cha habari au vyombo vya habari ili kueleza mikakati waliyonayo kuhusu eneo hilo hatarishi kwa wakazi Mkoani Katavi.
Eneo linalodaiwa kutokea ajali mara kwa mara lina makutanio ya barabara tatu za Mpanda-Sumbawanga,Mpanda-Kigoma na barabara inayoingia katikati ya mji ambapo mapaka sasa tangu barabara ikamilike hivi karibuni,kwa mjibu wa waendesha vyombo vya moto,zaidi ya ajali tano zimetokea katika eneo hilo na kusababisha vifo na majeruhi.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com ,au P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA