RAIS WA ZANZIBAR AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI WA TAASISI-Septemba 30,2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein,amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Shein amewateua Khamis Ramadhan Abdalla na Bibi Aziza Iddi Suweid kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar huku akimteua Kubingwa Mashaka Simba kuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Wengine ambao wameteuliwa ni George Joseph Kazi ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora anaeshughulikia masuala ya Katiba na Sheria pamoja na Kapteni Juma Haji Juma ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari.
Katika uteuzi wote huo ulioanza jana viongozi wa lioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu, Katibu waTume ya Maadili ya Viongozi na Naibu Makatibu Wakuu wa natakiwa kuripoti Ikulu siku ya Jumatatu tayari kwa kuapishwa

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA