MANISPAA YA MPANDA YASHINDWA KUPELEKA WAZEE DODOMA-Septemba 30,2017

Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
UMOJA wa wazee Mkoani Katavi umesema Manispaa ya Mpanda imeshindwa kuwezesha wazee ili kwenda kushiriki maadhimisho ya siku ya wazee duniani yanayofanyika kila ifikapo tarehe moja ya mwezi wa kumi.

Kwa mjibu wa makamu katibu wa umoja wa wazee Mkoani Katavi Bw.Nganyaga Mwendambali amesema,wakati huo huo,jioni ya leo wazee Mkoani Katavi wanatarajia kukutana kwa ajili ya kuzungumzia maadhimisho haya na kutoa sauti ya pamoja kuhusu maadhimisho hayo.
Awali kulikuwa na taarifa kuwa barua zinazota mwongozo kwa wakurugenzi kuwawezesha wazee washiriki maadhimisho zilichelewa kwa wakati ambapo hata hivyo haujajulikana ikiwa halmashauri zote tano za Mkoa wa wa Katavi zimeshindwa kupeleka wazee katika maadhimisho.
Kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 mkoa wa Katavi ulikuwa na wazee zaidi ya elfu tano.
Maadhimisho ya siku ya wazee Duniani,kitaifa kwa mwaka 2017 yanatarajiwa kuadhimishwa mkoani Dodoma na kauli mbiyu inasema ‘’Kuelekea uchumi wa viwanda tuthamini michango,uzoefu na ushiriki wa wazee kwa maendeleo ya taifa’’.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA