WILAYA YA MLELE YAZINDUA MKAKATI WA MAENDELEO WA MIAKA MITANO-Agosti 3,2017

Halmashauri ya wilaya ya Mlele mkoani Katavi imezindua mpango mkakati wa miaka mitano wa maendeleo ya mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2021.

Mpango mkakati huo umewasilishwa na afisa mipango wa halmashauri hiyo Bw. Afled Sungura wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika shule ya sekondari Inyonga siku ya jana.
Amesema mpango huo umefanyiwa tathimini katika ngazi ya vijiji, kata hadi halmashauri na baadhi ya mipango hiyo ni ujenzi wa soko la mazao ya kilimo, ujenzi wa hospitali ya wilaya, Ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa, ujenzi wa soko la bidhaa pamoja na ujenzi wa maegesho ya malori.
Nao baadhi ya madiwani wamesema wamepata taswira na dira ya maendeleo katika halmashauri yao.

Mpango mkakati huo unatarajia kugharimu zaidi ya shilling billion 8 na millioni 514 laki 885 na 530 ndani ya miaka mitano ijayo.   

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA