SHULE YA MSINGI NSAMBWE YAKABILIWA NA UPUNGUFU VYUMBA VYA MADARASA-Agosti 3,2017

Zaidi ya wanafunzi 250 wa shule ya msingi Nsambwe iliyopo kata ya Misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wanalazimika kusomea nnje k utokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Wakizungumza na mpanda radio baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema hali hiyo ni kikwazo katika maendeleo ya taaluma na kuiomba serikali kuchukua hatua za haraka. 

Mpanda radio fm imezungumza na baadhi ya walimu wa shule hiyo ambao wamegoma kuhojiwa  kwa madai ya kuogopa vitisho vya mamlaka ambayo hata hivyo hawakuwa tayari kuitaja. 

Mwaka 2015 uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ulitangaza kuanza mpango wake wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule hiyo ambayo mpaka sasa ina vyumba vya madarasa viwili tu  pamoja na ofisi ya walimu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA