WAZIRI WA AFYA MH.UMMY MWALIMU KUWASILI KESHO MKOANI KATAVI KUZINDUA ZOEZI LA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA-Agosti 15,2017

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
WAZIRI wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu anatarajia kuwasili kesho mkoani Katavi kwa ajili ya kuzindua zoezi la siku  tano la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

Mbunge wa viti maalumu Mkoani Katavi Anna Lupembe akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya polisi Mpanda amesema,timu ya madaktari bingwa wapatao 25 kutoka Dar es Salaam kutoka taasisi mbalimbali wamewasili Mkoani Katavi kwa ajili ya zoezi hilo.
Mkurugenzi wa taasisi ya kinga dhidi ya magonjwa sugu CCP Medicine ya Dar es Salaam Dk.Frank Manase pamoja na mambo mengine amesema,katika zoezi hilo lililoanza leo na kutarajiwa kufikia tamati Ijumaa ya wiki hii,wameambatana na taasisi  mbalimbali zikiwemo taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,Taasisi ya saratani ya Ocean road,madaktari kutoka chama cha kisukari Tanzania  na taasisi ya madaktari wa kinywa na meno na lengo likiwa ni kutoa huduma ya upimaji wa afya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Yahya Hussein amesema,pamoja na ukosefu wa vifaa vya kupimia magonjwa sugu Mkoani Katavi pia Mkoa wa Katavi una ukosefu wa madaktari bingwa wa magonjwa sugu ya wanaume huku kukiwa na madaktari bigwa wawili pekee wanaopima magonjwa ya wanawake.
Miongoni mwa Magonjwa sugu yanayopimwa ni pamoja na magonjwa ya moyo na saratani yakiwemo saratani shingo ya kizazi,kiharusi,shinikizo la damu la juu,saratani ya matiti na saratani ya tezi dume ambapo sababu kuu ya kuongezeka magonjwa hayo ni pamoja na tabia ya ulaji kutofanya mazoezi, kutokuwa desturi ya kupima afya mara kwa mara na uvutaji wa sigara.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com

Barua pepea:p5tanzania@gmail.com,Mawasiliano 0764491096

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA