SERIKALI YA MTAA MKOANI KATAVI YAHOFIA MAFURIKO YA WANAFUNZI-Agosti 12,2017

SERIKALI ya mtaa wa Kampuni kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,Imeiomba Manispaa ya Mpanda kuandaa miundombinu ya madarasa ya kutosha katika shule ya msingi Nsambwe,ili kukidhi idadi ya wanafunzi itakayoongezeka katika shule hiyo baada ya wakazi wa mtaa wa msasani na tambukareli kuhamia eneo hilo wakiwa na wanafunzi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Kampuni Bw.James Simon amesema,vyumba viwili vya madarasa vilivyopo katika shule ya msingi Nsambwe haviendani na idadi ya wanafunzi takribani 300 waliopo huku baadhi yao kati ya hao hulazimika kusomea nje.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Nsambwe Bw.Joseph Mayala amesema Shule ya Msingi Nsambwe iliyoanzishwa mwaka 2015 kwa sasa ina wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tano na walimu watatu ambapo amesema kama hakuna vyumba vingine vya madarasa vitavyojengwa hali itakuwa mbaya zaidi hasa msimu wa mvua.

Zaidi ya kaya 300 za mtaa wa Msasani watakaobomolewa makazi yao na shirika la Reli Tanzania TRL ifikapo mwezi Januari mwakani ili kupisha mipaka ya hifadhi ya reli Wilayani Mpanda wanatarajia kuhamia katika mtaa wa kampuni hali itakayopelekea ongezeko la idadai ya wanafunzi na kuleta changamoto

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA