RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI,WAMO WAWILI WA VYUO VIKUU,MWENYEKITI WA KAMPUNI YA KUHIFADHI MAFUTA,MWENYEKITI WA BARAZA LA USHINDANI -Agosti 18,2017



Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli,amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa chuo kikuu cha Ardhi.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es salaam inasema Rais Magufuli amemteua Prof. Evaristo Liwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, kuchukua nafasi ya Prof. Idrissa B. Mshoro ambaye amestaafu.
Wakati huo huo Rais Magufuli amewateua Prof. Abdulkarim Khamis Mruma kuwa Mwenyekiti wa kampuni ya kuhifadhi mafuta (TIPER), ambaye kabla ya kuteuliwa alikuwa ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Jiologia Tanzania,na Prof.Joseph Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania LTD.
Prof.Buchweshaija alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam  (DUCE).

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amemteua Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal - FCT).
Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Zainab Goronya Muruke ambaye amemaliza muda wake.
Kabla ya uteuzi huu Mhe.  Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.
Wajumbe wa Baraza la Ushindani ni;
1.   Mustafa Siyani
2.   Donald L. Chidowu
3.   Susana Mkapa
4.   Bibi Bitamo Kasuku Phillip
5.   Yose Joseph Mlyambina
6.   Dkt. Theodora Mwenegoha
Uteuzi huu umeanza  tarehe 18 Agosti, 2017

 Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA