MADAKTARI BINGWA KUTOKA DAE SES SALAAM WATOWEKA BILA TAARIFA KWA WAGONJWA MKOANI KATAVI,WAGONJWA WAHAHA KUPATA MATIBABU,MGANGA MKUU MKOA WA KATAVI ASHIKWA KIGUGUMIZI KUSEMA HALI ILIVYO-Agosti 18,2017

Mh.Anna Lupembe Mbunge viti Maalumu Katavi(PICHA na.Issack Gerald)
WAGONJWA ambao wamewasili  Mjini Mpanda wakitokea maeneo mbalimbali Mkoani Katavi kwa lengo la kupimwa na kutibiwa na madaktari bingwa wameeleza kusikitishwa na hatua ya madaktari hao kuondoka ghafla bila kutoa taarifa hatua ambayo imesababisha wagonjwa kupoteza muda na gharama za usafiri.


Hali hiyo imeibuka leo katika viwanja vya polisi Mpanda baada ya wagonjwa kuwasili katika viwanja vya polisi tangu alfajili na hatimaye kutowaona madaktari wanaotakiwa kuwapima na kuwatibu ambapo wameiomba serikali kuhakikisha madaktari wanajipanga kabla ya kuja kutoa huduma.
Baadhi ya wagonjwa wakiwa wamekata tamaa kutokana na hali kutoeleweka pamoja na mambo mengine wakaeleza ya moyoni mwao.
Hata hivyo Kutokana na hali hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Yahya Hussein amefika kutoa ufafanuzi mbele ya wagonjwa zaidi ya 100 waliokuwepo ambapo hakutaka kurekodiwa na chombo cha habari wakati akizungumza na hatimaye kusema chanzo cha madaktari kuondoka ni uhaba wa dawa.
Jumanne ya Wiki hii Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mh.Ummy Mwalimu alizindua zoezi la Siku tano la upimaji wa magonjwa Sugu ambapo juzi na jana akiwa Wilayani Tanganyika na Mlele aliwahamasisha wakazi kujitokeza kwa wingi kupatiwa matibabu.
Wakati huo huo,mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi Mh.Anna Lupembe aliyekuwa akiratibu zoezi zima la kuleta madaktari hao mkoani Katavi alipotafutwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa ya simu ili atoe ufafanuzi wa hali ilivyo juhudi hazikufanikiwa hata simu yake licha ya kuwa hewani haikupokelewa ambapo hata Mkurugenzi wa Taasisi ya CCP ya Dar es Salaam inayohusika na kudhibiti magonjwa sugu Dkt.Frank Manase ambaye naye alikuwa akiongoza masafara wa madaktari bingwa 25 naye pia hakupokea simu alipotafutwa
Miongoni mwa magonjwa sugu yaliyokuwa yanapimwa na mengine kutibiwa ni pamoja magonjwa ya moyo ikiwemo Shinikizo la damu na magonjwa ya saratani ikiwemo saratani ya mlango wa shingo ya kizazi saratani ya matiti saratani ya tezi dume na ugonjwa wa kisukari.
Jumla ya madaktari bingwa 25 kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete taasisi ya Saratani ya Ocean Road na taasisi zinazoshghulikia matatizo ya meno zilikuwepo kuendesha zoezi la siku tano la kupima na kutibu wagonjwa ambapo hata hivyo wametumia siku tatu badala ya siku tano huku mamia ya wakazi mkoani Katavi wakikosa kupimwa na kutibiwa.

Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA