HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA EKARI 2400 KWA AJILI YA UWEKEZAJI,SEKTA YA UFUGAJI,KILIMO,BIASHARA,UTALII,HUDUMA ZA JAMII NA MAKAZI YA WATU KUPEWA KIPAUMBELE-Agosti 21,2017

HALMASHAURI ya wilaya ya Mpanda mkoani katavi imesema  imetenga eneo la Luhafwe lenye ukubwa wa  ekari  2400  kwa ajili ya uwekezaji.

Hatua hiyo imebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Rojas Romuli wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema mikakati iliyopo kwa sasa  ni pamoja na kupima  viwanja kwa ajili makazi huku kwa kila kaya itapewa hekari mbili kwa ajili ya kilimo.
Aidha Romuli amesema lengo kuu ni kuhifadhi Ardhi na mazingira na kuyatumia katika namna ambayo ni endelevu kwa matumizi ya vizazi vya sasa na baadae.
Vipaumbele vilivyobainishwa katika uwekezaji huo ili kufikia kaulimbiu ya Tanzania ya Viwanda ni  pamoja na ufugaji,kilimo,utalii,huduma za kijamii,biashara pamoja na makazi ya watu.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli imekuwa ikiziagiza Halmshauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji ili kujenga Tanzania ya viwanda.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA