MKUU WA WILAYA YA MPANDA ATAKA WANANCHI WASIUZE CHAKULA OVYO KUEPUKA BAA LA NJAA-Julai 30,2017

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi. Lilian Charles Matinga ametoa wito kwa wananchi wilayani Mpanda kutunza chakula walichovuna katika msimu huu ili kujiepusha na baa la njaa linaloweza kujitokeza.

Matinga ametoa wito huo katika baraza la nne la madiwani wa halmashauri wa manispaa ya Mpanda lililofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa manispaa ya mpanda.
Amesema katika msimu huu wilaya ya Mpanda imezalisha chakula cha kutosha na hivyo ni jambo la aibu endapo wananchi watalalamika kukumbwa na njaa na badala yake wauze chakula cha ziada badala ya kuuza chakula cha familia.
Mkutano huo wa baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda wa kufunga mwaka wa fedha 2016/2017 ulitanguliwa na mkutano wa kawaida uliofanyika Alhamisi ya wiki mkutano ambao ulikuwa unatoa nafasi kwa madiwani kutoa taarifa za kila kata.

Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA