HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA ENEO LA UJENZI SHULE SEKONDARI YA KATA YA KASEKESE-Julai 30,2017

Mkuu wa Wilaya Tanganyika Salehe Mhando akisaini katika daftari la wageni 
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,imetenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata katika kata ya kasekese wilayani humo. 

Akizungumza na wananchi wa kata ya Kasekese  wakati akizundua kampeni ya hamasa kwa wananchi kujiunga na huduma ya mfuko wa afya ya jamii CHF mkuu wa wilaya ya  Tanganyika Salehe Mbwana Muhando amewapongeza wananchi kwa kutenga eneo zuri kwa ajili ya ujenzi huo.
Amesema serikali inaagiza kila kata kuwa angalau na shule ya sekondari moja hivyo amewaomba wananchi wa kata hiyo kushiriki katika ujenzi huo huku akichangia mifuko 50 ya simenti na akitarajia katika mwaka ujao shule hiyo ifunguliwe na wanafunzi waanze kusoma.
Kwa upande wake Afisa elimu sekondari  wilaya ya Tanganyika Bw. Michael William Nyambile   amesema eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari linatosha na angependa kuona ujenzi wa  miundombinu ya awali ya shule hiyo.
Kwa upande wao wananchi wa kata ya Kasekese wamepongeza hatua hiyo na kuwaomba wananchi wenzao kushiriki katika ujenzi huo ili watoto wao wapate elimu karibu.

Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA