MADEREVA WA MAROLI MKOANI KATAVI WAGOMA KUONDOKA UWANJA WA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MPANDA

MADEREVA  wanaoegesha magari katika uwanja wa shule ya msingi Mpanda iliyopo Halmshauri ya Manispaa ya Mpanda wamegoma  kutii agizo la kuondoka katika eneo hilo.

Wakizungumza na wanahabari  kwa mashariti ya kutotaja majina wamesema kuwa hawana taarifa yoyote kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa  ya Mpanda inayowataka kuondoka katika eneo hilo kwa madai wapo kihalali.

Mpanda radio fm imeshuhudia risiti yenye nembo ya Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda  zinazotolewa kwa malipo ya shilingi 1000 kama sehemu ya malipo katika eneo la uwanja wa shule hiyo.

Wiki iliyopita mkurugenzi Mtendaji wa manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu akihojiwa kwa njia ya simu na Mpanda radio alikanusha kuhusika na tozo katika uwanja huo na kuwataka madereva hao wawe wameondoka ifikapo jully 15 mwaka huu.

Habarika zaidi kupitia p5tanzania.blogspot.com

Mawasiliano :p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA