JESHI LA POLISI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI LATAKA ULINZI NA USALAMA UANZIE KATIKA FAMILIA-Julai 23,2017

JESHI la polisi Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,limewataka wananchi kuhakikisha ulinzi na usalama vinaanzia katika familia.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Polisi Wilayani Mpanda Maria Dominick,katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Mpanda Hotel ambapo kwa upande wake mkuu wa Usalama barabarani Wilayani Mpanda Inspekta Lazaro Masembo ameonya matumizi ya vilevi kwa madereva wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.
Katika hatua nyingine,wanaume wametakiwa kuacha tabia ya kutelekeza wake na familia kwa ujumla kwa kuwa tabia hiyo inasababisha kuongezeka kwa ugumu wa maisha katika familia
Baadhi ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilayani Mpanda,akiwemo Oscar Mbuye wa mtaa wa Tambukareli wamesema wamekuwa wakipokea kesi nyingi zinazohusisha wanawake kutelekezwa na waume zao huku wanaume hao wakidaiwa kutumia ovyo pesa walizonazo nje ya familia.

Habari zaidi ni P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA