WAKAZI KITONGOJI CHA KAMINI HALMASHAURI YA NSIMBO WAOMBA OPARESHENI YA KUWAONDOA KATIKA ENEO LA HIFADHI ISITISHWE.



Na.Issack Gerald-Mpanda-Januari 30,2017
WAKAZI wa kitongoji cha Kamini kilichopo kata ya Ugalla wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamwasilisha barua katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiomba Oparesheni ya kuwaondoa katika kitongoji hicho isitishwe kwa madai kuwa mipaka kati ya kitongoji hicho na misitu ya hifadhi haikufuata taratibu na mipaka kukosewa.

Akizungumza kwa masikitiko Bw Edward Labati Amala ambaye amewasilisha barua hiyo kwa niaba ya wananchi wenzake amesema zoezi la kuwaondoa baadhi ya wakazi walio katika miliki ya hifadhi limefanyika kabla ya kufanyika mkutano wa kijiji uliotarajiwa kufanyika Januari 29 mwaka huu ukishirikisha viongozi kutoka idara ya misitu Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Aidha amesema uharibifu wa mali za wananchi ni mkubwa katika Oparesheni hiyo ambapo hata hivyo wananchi hao wameomba wapewe nafasi ya kutunzana kuvuna mazao ambayo yamelimwa na wakazi hao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ugalla Mh Halawa Charles Malengeja pamoja na kusikitishwa na oparesheni hiyo kufanyika kabla ya mkutano wa kijiji kama ilivyokuwa imepangwa tangu Januari 8 mwaka huu pia amesema hana taarifa rasmi kutoka Halmashauri juu ya oparesheni hiyo iliyoanza Januari 24.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw. Mwailwa Smith Pangani licha ya kusema kuwa atakapopokea barua ya wananchi hao ataipitia na kuitolea maamuzi pia amesema Oparesheni ya kuwaondoa baadhi ya wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi haitasitishwa.
Aidha Bw Pangani amesema Oparesheni hiyo iliyoanza Januari 24 mwaka huu itachukua siku 10 ambapo wakati huo huo ametoa wito kwa wakazi hao wanaoondolewa katika eneo hilo kihamia katika kijiji cha Katambike ambapo kuna maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao.
Januari 8 mwaka huu,Mbunge wa jimbo la Nsimbo Mh.Richard Mbogo alifany amkutano wa hadhara katika kitongoji cha Kamini na kupokea kero hizo za wananchi ambapo ndiye aliyeuagiza uongozi wa kitongoji kwa kushirikiana na wataalamu wa misitu wafanye mkutano januari 29 kabla ya oparesheni kufanyika tukio ambalo limekwenda tofauti na ilivyokuwa imepangwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA