WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWASILI KATAVI KESHO,WANAKATAVI WAOMBWA KUJITOKEZA KUMPOKEA.



Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga  ametoa rai kwa wananchi Mkoani Katavi kujitokeza kwa wingi kumpokea waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa anayetarajia kuwasili kesho kwa ndege Mkoani Katavi kwa Ziara ya kikazi ya siku nne.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald)
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majliwa(PICHA NA.Issack Gerald)
                                         

Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maandalizi ya kumpokea waziri Mkuu mkoani hapa.
Waziri Mkuu akiwa Mkoani Katavi,atafanya mikutano mbalimbali ya Hadhara katika Wilaya za Mkoa wa Katavi ikiwemo kutembelea kijiji cha Majalila kunakojengwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika na Draja la mto Kavuu lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Kabla ya Waziri Mkuu kuhitimisha Ziara Agosti 26 mwaka huu akiwa Mkoani Katavi na kurejea Dar es Salaam,Agosti 23 siku ya Alhamisi anatarajia kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Rukwa.
 Katika hatua nyingine kutokana na tetesi za baadhi ya wanakijiji wa vijiji vilivyopo mbali na kijiji cha Majalila kilichopo Kata ya Tongwe kutangazwa kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kuanza kulalamika kwamba huenda wakakosa baadhi ya huduma kutokana na umbali waliopo,Mkuu wa Mkoa kupitia Meja Jeneral Muhuga akitolea ufafanuzi kuhusu kijiji cha Majalila kuwa makao makuu amesema kuwa ni maamuzi yalitokana na vikao mbalimbali vilivyofanyika kwa nyakati tofauti vikiwemo vikao vya balaza la madiwani na vikao vya kamati ya ushauri ya Mkoa.
Aidha pamoja na mambo mengine,mkuu wa Mkoa amesema maamzi yalifanyika ili kumaliza mvutano juu ya makao makuu yanakotakiwa kuwa na kuondoa vizingiti vya shuhuli zamaendeleo.
Kijiji cha Majalila kilitangazwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Agosti 4 mwaka huu.
  
 RATIBA KAMILI YA ZIARA YA WAZIRI MKUU KATAVI-RUKWA
20-8-2016- WILAYANI MPANDA
-Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili jioni uwanja wa ndege
21-8-2016 HALMSHAURI YA WILAYA YA NSIMBO(WILAYANI MLELE)
Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea Ofisi za CCM Mkoa wa Katavi,Atafanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ndui Staion yaliyokuwa makazi ya wakimbizi Katumba pamoja nakuzindua mnara mpya uliojengwa na watanzania wapya wa hapo Katumba kama pongezi kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwapatia uria.
-Waziri Mkuu atafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya Msingi Azimio.

22-8-2016 WILAYANI MLELE
- Waziri Mkuu ataanza ziara katika Wilaya ya Mlele na kuongea na watumishi,kupata taarifa ya mkoa na kufanya mkutano wa Hadhara.
- Waziri Mkuu atarejea Ikulu Mpanda Mjini
- Waziri Mkuu  taelekea Kijiji cha Majalila Makao Makuu ya halmshauri na Wilaya Mpya ya Tanganyika
- Waziri Mkuu  ataona mradi wa maji majalila
- Waziri Mkuu  atafanya mkutano wa hadhara katika kata ya Mpanda ndogo kasha
-Atarudi Mpanda Mjini Ikulu.

23-8-2016 WILAYANI MPANDA
-Waziri mkuu atafanya mkutano katika ukumbi wa idara ya Maji ikiwa ni majumuisho ya ziara mkoani Katavi
-Baada ya hapo ataelekea Majimoto Wilayani Mlele katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambapo atafanya mkutano wa hadhara.
-HATIMAYE ATAELEKEA MKOANI RUKWA KUENDELEA NA ZIARA MKOANI KUANZIA AGOSTI 23-26,2016.

WILAYANI MLELE-26-8-2016
-Waziri Mkuu atarejea Mkoani Katavi kuonana na waziri Mkuu Mstaafu katika kijiji cha Kibaoni.
-Baada ya mazunumzo na Waziri Mkuu Mstafu,Waziri Mkuu atatembelea shule mpya ya msingi Kakuni.
NA HATIMAYE ATAREJEA MPANDA MJINI KUPANDA NDEGE KUELEKEA DAR ES SALAAM.
Endelea kuhabrika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA