WATANO KATAVI WAHUKUMIWA MIAKA 5-20 KWA TUHUMA ZA NYARA ZA SERIKALI,MWINGINE AACHIWA HURU,WAKILI WAO ASEMA WATAKATA RUFAA



Na.Vumilia Abel-Mpanda
MAHAKAMA ya wilaya mkoani Katavi imewahukumu watu 5 miaka 5 hadi 20  na mmoja kuachiwa huru waliokuwa wakikabiliwa na  makosa matatu tofauti likiwemo la kukutwa na nyara za serikali bila kibali.

Akisoma hukumu hiyo hakimu Chingangwa Tengwa amewataja washtakiwa hao kuwa ni Justini Baluti,Boniface Hoza,Elias Hoza,Credo Gervas na Sadock Masamba.
Ameongeza kuwa kosa la kwanza ni kujihusisha na makosa ya uhujumu uchumi,pili ni kukutwa na nyara za seikali bila kibali na kosa la tatu linamhusu mshtakiwa Boniface Hoza aliyekutwa na nyara za serikali vipisi 7 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya sh.milioni mia moja.
Kufuatia hatua hiyo  mahakama imewakuta na hatia washtakiwa wanne waliokuwa wakikabiliwa na kosa la kukutwa na nyara za serikali vipande 15 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 249 ambao wote watatumikia kifungo cha miaka mitano jela .
Aidha Chigangwa amesema kwa kosa la pili mahakama imewakuta na hatia washtakiwa Jastini Baluti na Boniface Hoza wote watatumikia kifungo cha miaka ishirini jela.
Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa serikali Bw.Wankyo Simon aliomba mahakamani hapo kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa watu wenyingine.
Nje ya mahakama baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa serikali Simon amesema ameridhishwa na maamuzi yaliyotolwa na mahakama kama hapa anavyoeleza
Naye wakili upande wa utetezi uliosimamiwa na Bw.Elias Kifunda amesema kwa kuwa washatkiwa hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama wanatarajia kukata rufaa.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA