WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUANZA ZIARA KATAVI JUMAMOSI HII,KUTEMBELEA MAJIMBO YOTE MATANO YA MKOA WA KATAVI,SEHEMU YA RATIBA P5 TANZANIA IMEKUSOGEZEA HII HAPA



Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Katavi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa
                                       

Mh.Richard Mbogo(mbunge) Jimbo la Nsimbo katika mahojianiano na waandishi wetu wa habari,amesema kuwa Waziri mkuu akiwa Mkoani Katavi anatarajia kutembelea jimbo La Katavi linaloongozwa na mbunge Issack Kamwele (CCM),Jimbo la Kavuulinaloongozwa na  mbunge Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM)Mpanda Mjini linaloongozwa na mbunge Sebastian Kapufi (CCM),Jimbo la Mpanda Vijijini linaloongozwa na mbunge Moshi Selemani Kakoso (CCM) na Jimbo la Nsimbo linaloongozwa na mbunge Richard Mbogo (CCM).
Mh.Mbogo amesema Waziri Mkuu Kassim mara baada ya kuwasili Mkoani Siku ya Jumamosi Tarehe 20 ataanza ziara rasmi siku ya Jumapili Tarehe 21 ambapo ataanzia Jimbo la Mpanda Vijijini kwa kufanya mkutano majira ya asubuhi katika kijiji cha Majlila,Jimbo la Nsimbo atafanya mkutano katika Kijiji cha Nduwi Station majira ya Mchana na mkutano wa tatu utafanyika mkutano Mpanda Mjini katika viwanja vya Shule ya Msingi Azimio.
Baada ya mikutano hiyo ataendelea na ziara katika majimbo ya Kavuu,Mpimbwe na Katavi.
Mapema mwezi Februari,20 mwaka huu kulifanyika kongamano  la Maendeleo ya Rukwa na Katavi lilifanyika Jijini Dar es salaam katika viwanja vya Makumbusho ambapo akiwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliahidi kuisaidia mikoa ya Rukwa na Katavi kujikwamua katika Shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mpaka kufikia sasa kwa mwaka 2016,takribani Mawaziri wane wamefanya ziara katika Mkoa wa Katavi kusikiliza kero za wananchi,kuzungumza na wadau mbalimbali wa maendeo,kukagua miradi ya maendeleo na mengine kuyawekea mawe ya msingi pamoja na kutoa maagizo kwa viongozi Mkoani Katavi kufanya utekelezaji wa kiutendaji katika shughuli mbalimbali.
Miongoni mwa Mawaziri ambao wametembelea Mkoani Katavi ni pamoja na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Mwigulu Lameck Nchemba.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM,Usikose kitakochoendelea katika ziara ya Waziri Mkuu

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA