AFISA MTENDAJI WA KIJIJI APEWA WIKI MBILI KUWAONDOA WAKAZI WALIOVAMIA MISITU NA KUFANYA MAKAZI,MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA PIA AZUNGUMZIA ZIARA YA WAZIRI MKUU KATIKA WILAYA YAKE



Na.Issack Gerald Bathromeo
MKUU wa wilaya ya Tanganyika Saleh Muhando ametoa wiki mbili kwa Afisa mtendaji wa kijiji cha Mpembe kata ya Katuma kuhakikisha anawaondoa wananchi waliovamia misitu na  kufanya makazi.

Ametoa agizo hilo leo kufuatia uharibufu  mkubwa wa mazingira uliofanywa na wananchi kwa kufanya shughuli za ukataji miti,uchomaji mkaa na kilimo.
Bw.Mhando amesema ni wajibu wa kila mwananchi kutunza mazingira ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na uharibifu huo.
Ameongeza kusema kuwa mwananchi yeyote ambaye atakaidi agizo hilo sheria itachukuwa mkondo wake.
Wakati huo huo amewaasa wakazi wa Wilaya ya Tanganyika kujitokeza kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akapoanza ziara katika Wilaya hiyo Jumapili Agosti 21 mwaka huu.
Aidha amesema kuwa anajisikia furaha Waziri Mkuu kuanzia ziara katika Wilaya hiyo mara baada ya kuwasili Mkoani Katavi ambapo anatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Majalila kunakojengwa makao makuu ya Wilaya hiyo change kabisa.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM,Usikose kitakochoendelea katika ziara ya Waziri Mkuu

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA