UNHCR WATOA MSAADA WA GARI LA MILIONI 78,732,000 KITUO CHA AFYA MISHAMO,WANANCHI HALMSHAURI WATAKIWA KULITUNZA NA KULITUMIA KATIKA MALENGO HUSIKA



Na.Issack Gerald Bathromeo
Shirika la kimataifa linalojishughulisha na kusaidia wakimbizi duniani UNHCR,limetoa msaada wa gari la wagonjwa kwa kituo cha afya cha Mishamo kilichopo kata ya Mishamo tarafa ya Mishamo Wilaya Mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akiwasalimia wagonjwa katika kituo cha afya cha Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 5,2016
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando mwenye suti nyeusi akizungumza na (katikati) ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mishamo.Mkuu wa kituo Polisi Mishamo anaitwaOCS Ispecta MatongoMashaka na aliye kulia ni Afisa wa upelelezi Wilaya ya Tanganyika(PICHA NAIssack Gerald)Agosti 5,2016
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akitoka ndani ya Kituo cha afya Mishamo kusalimia wagonjwa(PICHA NAIssack Gerald)Agosti 5,2016
                                   

Akikabidhi gari hilo katika kituo cha afya cha Mishamo kwa niaba ya UNHCR,Wakili wa UNHCR kituo cha makazi mapya kwa watanzaia wapya waliokuwa wakimbizi Bw,Adolph Bishanga amesema gari hilo lenye thamani ya shilingi Milioni 78,732,000 limetolewa katika kituo hicho ili kuunga mkono serikali ya awamu ya tano ya kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa gari la wagonjwa katika kituo hicho cha afya.
Aidha ametoa rai kwa wananchi kilitunza vizuri huku akitaka Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika kutobadirisha matumizi ya gari hilo na badala yake litumike kwa matukio ya dharula hususani kwa wakazi wa Mishamo.
Amesema gari la awali lambalo lilitolewa na UNHCR mwaka 2012 mpaka sasa halijulikani lilipo baada ya Halmshauri kubadirisha kituo inapotakiwa kutoa huduma gari ambalo halikujulikana lilipo miezi mitatu tangu kukabidhiwa.
Bw.Bishanga amesema kuwa UNHCR litaendelea kushrikiana na serikali ya Tanzania kutatua changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya Afya na elimu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akipokea gari hilo na kulikabidhi kwa wananchi kupitia kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Ngalinda Hawamu Ahmada mbabli na kulipongeza Shirika la UNHCR kwa msaada huo,ametaka pia wananchi wa Mishamo na Wilaya ya Tanganyika kwa ujumla kulitunza vizuri gari hilo.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Ngalinda Hawamu Ahmada ametoa onyo kwa mtumishi yeyote kutotumia gari hilo kama daladala katika shughuli binafsi na atakayefanya hivyo atashughulikiwa kwa mjibu wa kanuni na taratibu.
Wakazi wa Kata ya Mishamo na wakazi wengine wote wanaotegemea kupata huduma ya gari hilo na katika kituo cha afya mishamo wamepongeza hatu ya UNHCR kutambu uhai na thamani ya wakazi wa Mishamo.
Katika ziara ya mkuu wa Wilaa aliyoifanya jana,aliambatana pia na wakuu wa idara mbalimbali wa afya wakiwemo Kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Dkt.Mhamed Mpunjo na Muuguzi Mkuu Wilaya ya Tanganyika.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPO.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA