MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AFUTA RASMI USHURU,YEYE NA MKURUGENZI WA HALMSHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA WAACHA NAMBA ZA SIMU KWA WANANCHI ILI WAPOKEE KERO ZA WANANCHI HATA KWA SIMU



Na.Issack Gerald Bathromeo
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Tanganyika  Saleh Mbwana Mhando ametangaza rasmi kufuta ushuru kwa fanyabiashara wadogo kwa wakazi wa Wilaya ya Tanganyika kama Rais wa Jamhuri ya Muungano alivyoagiza kufuta ushuru unaomkandamiza mwananchi.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Ipwaga wakimpokea Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando mara baadha ya kuwasili kijiji cha Ipwaaga(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 5,2016
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando akisaini katika kitabu cha wageni Kijiji Ipwaga(PICHA NA.Issack Gerald)Agost  5,2016
                          

Bw.Mhando ametangaza jana rasmi kufuta ushuru huo wakati akizungumza  na wakazi wa kata za Ipwaga na Mishamo alipofanya ziara ya kujitambulisha kwa wananchi na kusikiliza kero za wananchi wa kata hizo.
Amesema kuwa,wanaotakiwa kulipa ushuru ni wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa ajili ya baiasahara na siyo mkulima wa kawaida anayetoa mazao shambani kwenda kula au muuzaji wa bidhaa ndogondogo kama vile nyanya,mchicha,dagaa na bidhaa nyingine ndogondogo kwa ajili ya kujikimu kimaisha.
Aidha amesema kuwa mtoza ushuru wa aina yoyote aliyekuwa akitoza ushuru ni bora akafanye kazi nyingine ili kujiepusha kujiweka katika matatizo kwa serikali ya awamu ya tano imelenga kumsaidia mwananchi wa hali ya chini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika amesema ni wakati wa kutenda kuliko maneno kwa kuwa wananchi wanahitaji maendeleo na kusisitiza kuwa serikali haitamfumbia macho mtumishi wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika atakayekiuka kanuni za utumishi na maadili ya kazi yake anayotakiwa kuitekeleza.
Kwa upande wao wakazi wa  kata za Mishamo na Ipwaga  wakizungumza kwa furaha,wamepongeza Serikali ya Wilaya ya Tnaganyika na serikali ya awamu ya tano kwa kufuta ushuru unaomkandamiza mwananchi na kusema kweli serikali ya awamu ya tano imelenga kuwakomboa.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Salehe Mbwana Mhando na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Ngalinda Hawamu Ahmada wamewaachia namba za simu wananchi ili wazitumie kuwa pigia wanapoona kuna kero katika maeneo yao ikiwemo kero za viongozi wao kuwanyanyasa,kutopata huduma za jamii ipasavyo kama hospitalini na watendaji wote watakaotenda kinyume na kanuni za utumishi.
Hata hivyo wamesisitiza kutotumia namba hizo kuongea majungu isipokuwa watoe taarifa zenye ukweli ili zidfanyiwe kazi haraka na mwananchi yeyote atakayetoa taarifa za uongo pia naye atashughulikiwa kisheria.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPO.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA