KATIBU TAWALA MKOA WA KATAVI AAGIZWA KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA KUMHUSU AFISA MIPANGO MANISPAA YA MPANDA




Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wakandarasi wanaojenga stendi ya mabasi mpanda.(PICHA NA.Issack Gerald)
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi),Selemani Jafo ameendelea na ziara yake leo mkoani Katavi ambapo amemuagiza Afisa Tawala wa Mkoa wa Katavi kuunda timu ya uchunguzi ili  kuchunguza tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa Afisa Mipango miji wa Manispaa ya Mpanda ambapo anatuhumiwa kuchukua maeneo ya wananchi bila utaratibu.
Naibu Waziri Suleiman Jafo akiwa na walimu wa shule ya sekondari Kabunga(PICHA NA.Issack Gerald)
                                              

Jafo katika ziara hiyo ametembelea wilaya ya Tanganyika na wilaya ya Mpanda.
Katika wilaya ya Tanganyika aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Mpanda vijijini Moshi Kakoso ambapo alikagua  mradi wa Maktaba ya shule ya sekondari Kabunga pamoja na mradi wa Maji katika jimbo la mpanda vijiji.
Kwa upande wa Manispaa ya Mpanda alifanikiwa kukagua hospitali ya wilaya ya Mpanda pamoja na ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa.
Hata hivyo Jafo ilihitimisha kwa kufanya mkutano na watumishi wote wa Halmashauri ya Mpanda pamoja na Manispaa ya Mpanda katika  ukumbi wa idara ya maji uliopo mjini Mpanda.
Naibu Waziri ameendelea kutoa maelekezo ya utendaji kazi kwa watumishi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia dhana kubwa ya mabadiliko.
Katika majumuisho hayo, Jafo hakufurahishwa na tabia ya baadhi ya watumishi wenye tabia ya ubadhirifu wa fedha za umma na kutowajali wananchi.
Kuhusu Afisa mipango huyo, Jafo amesema amewapa fedha kidogo wananchi wenye ardhi nje ya utaratibu kisha kuyauza maeneo hayo kwa gharama kubwa kwa matajiri.
Kadhalika, Jafo amesema Afisa huyo analalamikiwa kuhodhi viwanja kadhaa ndani ya Manispaa hiyo kwa kutumia wadhifa alionao.
“Kutokana na tuhuma hizo namuagiza Katibu tawala mkoa(RAS) Katavi kuunda timu ya uchunguzi kisha kuwasilisha ripoti Ofisi ya Rais Tamisemi kwa hatua za kinidhamu endapo itabainika ukweli wa tuhuma hizi,”alisema Jafo.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA