WAZIRI MKUU WA INDIA KUWASILI LEO TANZANIA KUANZA ZIARA,SEKTA ZA VIWANDA,MAJI,ELIMU,SAYANSI NA TECHNOLOJIA KUPEWA KIPAUMBELE




WAZIRI Mkuu wa India, Narendra Modi anawasili leo nchini kwa ajili ya ziara ya kitaifa ya siku mbili kwa lengo la kudumisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
               

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga alisema Modi atatumia fursa hiyo kukuza uhusiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili pamoja na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi.
Alisema Modi atakutana na Rais John Magufuli Ikulu na kufanya naye mazungumzo.
Akiwa hapa nchini atasaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya sekta za viwanda, maji, elimu, sayansi na teknolojia na baadaye kuzungumza na waandishi wa habari.
Aidha Dk Mahiga alisema Modi pia atazungumza na jumuiya ya wafanyabiashara wakubwa wa India ambao baadhi yao wameshaonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya ujenzi wa viwanda vya kutengeneza chuma, saruji, dawa ya binadamu na maji ya matunda.
Kongamano hilo litakalowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali hapa nchini linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi huku Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Dk Augustine Mahiga akiwataka wafanyabiasha wa Tanzania kutumia fursa hii kushiriki ipasavyo ili waweze kukutana na wafanyabiashara wenzao.
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA