MWENGE WA UHURU KUWASILI KESHO MKOANI KATAVI,WANAKATAVI WAASWA KUDUMISHA AMANI



WANANCHI mkoani Katavi wametakiwa kudumisha amani na utulivu katika  kipindi hiki ambacho wanatarajia kupokea mwenge wa uhuru.
                                                 

Rai hiyo imetolewa   na Kaimu kamanda mkoa wa Katavi  Focas Malengo wakati akizungumzia kuhusu mandalizi ya upokezi wa mwenge wa uhuru unaotarajia kuwasili julai 10 mwaka huu.
Ameongeza kusema kuwa mwenge huo ukiwa mkoani  hapa unatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya  maendeleo.
Aidha ameeleza kuwa kilele cha mbio za mwenge kinatarajiwa kuwa julai 14 katika mkoa huu ambapo utaelekea mkoani Kigoma.
Mwenge wa uhuru ulizinduliwa Mkoani Morogoro Aprili 8 mwaka huu na Makamu wa Rais wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ambapo kilele chake kitahitimishwa Oktoba 14 Mkoani Simiyu.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni ‘’Vijana ni nguvu kazi ya taifa,Washirikishwe na kuwezeshwa’’

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA