WAKAZI KATAVI WAENDELEA KUCHAMBUA UTEUZI WAKURUGENZI WAPYA WAWASHAURI WAKURUGENZI KUTEKELEZA KAULI MBIU YA ‘’HAPA KAZI TU’’ IPASAVYO


Wakazi Mkoani Katavi wamesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uteuzi wa wakurugenzi alioufanya Julai 7 mwaka huu ni mzuri ikiwa walioteuliwa watafanya kazi kwa kuzingatia kiapo cha maadili na utumishi wa umma wanachoapa kabla ya kuanza kazi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli
                                                  

Wamesema kuwa  wakurugenzi walioteuliwa katika Halmashauri zilizopo Mkoani Katavi wamewsahauri kusimamia kwa misingi ya haki ili kuleta maendeleo ya wananchi.
Miongoni mwa wananchi ambao wametoa maoni ni pamoja na Askofu wa makanisa ya New Harvest Tanzania Askofu Laban Ndimubenya,baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vilivyopo Mkoani Katavi sanjari na wananchi wa kawaida.
Maoni hayo yametolewa ikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli Julai 7 mwaka huu ambapo wanatarajia kuapishwa siku ya Jumatatu Julai 12 mwaka huu.
Halmshauri za Mkoa wa Katavi zilizopata wakurugenzi wake ni pamoja na
 1.Mlele DC                               -           Alex Revocatus Kagunze
2.Mpimbwe DC                       -           Erasto Nehemia Kiwale
3.Mpanda DC                          -           Ngalinda Hawamu Ahmada
4.Mpanda Manispaa               -           Michael Francis Nzyungu
5.Nsimbo DC                           -           Joachim Jimmy Nchunda
Uteuzi wa wakurugenzi unahusisha halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa,65 waliteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani waliokuwa katika serikali ya awamu ya nne iliyokuwa ikiongozwa na Rais msitaafu wa awamu ya nne Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete huku wakurugenzi wakiwa wapya 120 wengi wao wakiwa vijana.
Wakurugenzi wameteuliwa siku chache baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya kuteuliwa Juni 26 mwaka huu ambapo wakuu wa wilaya katika Wilaya za Mkoa wa Katavi ni pamoja na
1.     Mlele            Rachiel Stephano Kasanda
2.     Mpanda            Lilian Charles Matinga
3.     Tanganyika            Saleh Mbwana Mhando
Wakuu hawa wa Wilaya tayari wamekwishaapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi mpya wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Raphael Mugoya Mhuga
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA