NEC YAKABIDHI RIPOTI YA TAARIFA YA UCHAGUZI KWA SERIKALI YA MKOA WA KATAVI


Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imeikabidhi serikali ya Mkoa wa Katavi ripoti ya taarifa ya uchaguzi wa udiwani,ubunge na urais uliofanyia mwaka jana Oktoba 25.
                                            

Akikabidhi ripoti hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi mbele ya waandishi wa habari,Afisa wa tume ya uchaguzi Taifa Bw.Peter Mwezi amesema,nakala za ripoti hiyo zitasambazwa katika ofisi zote za serikali zikiwemo Ofisi tatu za wakuu wa Wilaya waliopo mkoani Katavi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Mstaafu Jeneral Raphael Mugoya Muhuga pamoja na kuipongeza tume kwa kukamilisha uandaaji wa taarifa ya uchaguzi na kusimamia uchaguzi kwa amani na utulivu,amesema ripoti hiyo inatakiwa kusomwa na kubaini maudhui yake.
Katika makabidhiano hayo mbali na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa akiwemo Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishna Paul Chagonja na kaimu katibu tawala  Salumu Shilingi.
Naye Mratibu wa uchaguzi Mkuu wa udiwani,ubunge na Urais Mkoani Katavi uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015 ambaye pia ni kaimu katibu tawala mkoani Katavi Bw.Salumu Shilingi,akizungumzia kuhusu mwongozo wa sasa wa makabidhiano ya ripoti ya taarifa ya uchaguzi,pamoja na mambo mengine amesema kutokana na umuhimu wa nafasi ya vyombo vya habari katika jamii,makabidhiano ya taaifa kama hiyo yanatakiwa yafanyike mbele ya waandishi wa habari kama ambavyo imefanyika.
Juni 23 mwaka huu,tume ya taifa ya uchaguzi NEC chini ya Mwenyekiti wake Jaji mstaafu Damian Lubuva,ilimkabidhi ripoti ya taarifa ya uchaguzi huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
 Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA