WAISLAMU KATAVI WAJIAANDA MFUNGO WA RAMADHANI,WANAKATAVI WAPEWA NENO



Leo ni siku ya mwisho ya siku ya Shaabani katika dini ya kiislamu ikimaninisha siku ya mwisho kabla ya mfungo wa siku ya ramadhani kuanza hapo kesho.

Wakati sikukuu hiyo ikitarajia kuanza kesho,Waislamu Mkoani Katavi wameaswa kutenda yaliyo mema sanjari na kusaidiana katika shida mbalimbali katika mfungo wa Sikukuu ya ramadhani unaotarajia kuanza kesho.
Ujumbe huo umetolewa na Shekh wa Mtaa wa Makanyagio na Imamu wa msikiti Mpanda Hotel ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Mashehe mkoa wa Katavi Sheikh Said Haruna Omary kwa lengo la kuzungumzia sikukuu hii ikiwa pia ni kutoa ujumbe kwa waumini wa dini ya kiislamu mkoani Katavi.
Miongoni mwa mambo ambayo amesisitiza ni pamoja na kusoma zaidi Quran,kusaidia wenye shida mbalimbali na kutofanya uharifu.
Halikadhalika baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiwemo Fatma Basesa mkazi wa Mtaa wa Makanyagio na Ramadhani Shabaani Makame ambao ni miongoni mwa waumini wa dini ya kiislamu pamoja na mambo mengine wamesema,watanzania wanatakiwa kudumisha amani kipindi cha ramadhani na kuzingatia mema yaliyofundishwa na mtume mahamad Suraray waray wasalaam.
Suala la bei za bidhaa nazo zimezungumza na baadhi ya waislamu huku wakitaka bei kutopandishwa kwani itakuwa kuwaumiza baadhi ya wasiokuwa na uwezo.
Mfungo wa ramadhani ni miongoni mwa nguzo kuu tano za dini ya kiislamu.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA