KATAVI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA,NDANI YA MIEZI 6 WATOTO ZAIDI YA 30 WAFANYIWA UKATIRI KATAVI



Mkoa wa Katavi umeadhimisha maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika   ambapo maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.

Watoto waishio katika mazingira magumu na walemavu wakizungumza katika maadhimisho hayo,wameiomba jamii kupinga ukatili wa kijinsia  dhidi yao kwani wanaathirika kisaikolojia na kudidimiza  ndoto zao .
Akisoma risala mbele ya mgeni rasimi  katibu wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoani Katavi  Bw George Charles amezitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya ulawiti,ubakaji ,ukosefu wa miundombinu  rafiki kwa walemavu mashuleni pamoja na mitazamo hasi juu ya watoto wenye ulemavu.
Kwa upande  msemaji  wa dawati la  jinsia na watoto  katika kituo cha polisi  mpanda  H 311 DC  Emanueli Lindege amekiri kuwepo kwa matukio ya ulawiti na ubakaji kwa watoto ambapo kuanzia mwezi January hadi juni kumeripotiwa na matukio ya ubakaji wa watoto zaidi ya 30.
Naye mgeni rasimi Bi.Josephina Chilongozi ambaye ni mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu  ameiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwa watoto waishio katika mazigira magumu na walemavu ambapo pia amewaasa watoto  kutoa taarifa kwa wazazi wao wanapokutana na vitendo vya kikatili.
Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika mjini  Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Ummy Mwalimu.
Siku ya mtoto  wa afrika  iliidhinishwa mwaka 1991 juni 16  ili  kuwaenzi watoto wenzao waliofariki kwa kupigwa risasi huko Soweto sauth afrika mauaji hayo yakiwa yametokea mwaka 1979 kwakipinga ubaguzi wa rangi.
Maadhimisho haya ya mwaka huu yametumia kauli mbiu isemayo ‘’ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo unaepukika chukua hatua kumlinda mtoto.’’
Mwandishi :Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA