JERA MIEZI 6 MPANDA AKITUHUMIWA KUJIPATIA FEDHA KWA UDANGANYIFU



Mahakama ya mwanzo mjini mpanda imemhukumu mtu mmoja kwenda jera   miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki mbili kwa kosa la kujipatia  fedha kwa  njia ya udanganyifu.

Akisoma  hukumu hiyo  hakimu  mkazi  Mh.Ramadhani Mkumbi amemtaja mshitakiwa kuwa ni  Joseph Lukasi  mkazi wa Nsemluwa manispaa ya Mpanda
Amsema kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo  mnamo Juni 20  mwaka huu   maeneo ya Mpanda hoteli na  kujipatia kiasi cha  zaidi ya   shilingi  Milioni tatu   fedha ya Bw.felix Makombe  mkazi wa majengo ambapo alidai kuwa alichukua fedha hiyo kwa lengo la kumununulia gunia 70 za mpunga lakini alitokomea na fedha hiyo pasipojulikana kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi.
Kufatia hatua hiyo mahakama imemhukumu  mtuhumiwa ili iwe fundisho  kwa watu wenye tabia kama hiyo.
       
Wakati huo huo mtu mwingine amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la wizi.
 Akisoma shitaka hilo  mwendesha mashitaka wa jeshi la police  PCL mtei  mbele ya hakimu mwandamizi  David Mbembela, amemtaja mshitakiwa kuwa ni Husseni Omari(12) mkazi wa Nsemluwa.
Amesema kuwa mnamo Mei 9 mwaka huu maeneo ya Kichangani tarafa ya kashaulili,mshitakiwa aliiba godoro moja futi 5 kwa 6 aina ya komfy,shuka mbili zenye thamani  ya shilingi elfuThelathini na pesa tasilimu  Laki laki moja na elfu sitini vyote  vikiwa na thamani ya shilingi Laki tatu na elfu sitini .
Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka hilo   na yupo nje kwa dhamana mpaka hapo  kesi itakapotajwa tena Juni 30 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa. 
Mwandishi :Ester Lameck
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo 
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM




Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA