AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI 6 KWA UBADHIRIFU WA FEDHA



Mahakama ya mwanzo mjini Mpanda imemhukumu mtu mmoja kifungo cha nje miezi sita kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka kwa kutumia fedha bila kufuata utaratibu wa ofisi.

Akisoma hukumu hiyo,hakimu mkazi Mh.Sylivester Makombe,amemtaja mshtakiwa kuwa ni Enjoy Juniour(21)mkazi wa Makanyagio,ambaye anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Mei  mosi mwak huu wakati akitoa huduma katika banda la Tigo-Pesa Mpanda Mjini.
Mh.Makombeamesema Bi.Enjoy alitumia zaidi ya Shilingi milioni mbili kwa matumizi yasiyoeleweka ambapo kwa upande wake mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo mara baada yak up[ewa nafasi ya kujitetea na ameomba kupunguziwa adhabu.
Hata hivyo mahakama imekubali kumpunguzia adhabu ambapo pia imesema itaendelea kutoa adhabu kali kwa watu wenye tabia kama hiyo ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mgira Magembe(27) mkazi wa Mpanda Hotel amefikishwa katika mahakama ya mwanzo kwa kosa la wizi wa baiskeli ina ya Sports yenye thamani ya shilingi laki moja na nusu iliyokuwa imekodiwa na Mariam Willium mkazi wa Kigambo.
Mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi Wilayani PC Mtei amesema kuwa tukio hilo limetokea leo Juni Mosi majira ya saa 12 asubuhi,katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo ambapo ameiambia mahakama kuwa baiskeli hiyo ameichukua kwa maelekezo ya rafiki akijua kuwa ndiye mmiliki.
Mshtakiwa amepelekwa mahabusu baadaya kukosa kukidhi vigezo vya dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 15 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya mlalamikaji.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA