WIZI WA SHUKA,GODORO NA FEDHA VYAMFIKISHA MAHAKAMANI MPANDA



Mtu mmoja mkazi wa kata ya Nsemulwa Wilayani Mpanda amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo Mjini Mpanda kwa kosa la wizi wenye vitu vyenye thamani ya kiasi cha zaidi  ya shilingi laki tatu.

Akisoma shitaka hilo jana,mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi  PC Mtei  mbele ya hakimu mwandamizi Bw.Davi Mbembela amesema mnamo tarehe 9 mei majira ya saa 10 usiku mshtakiwa  Huseni  Omary mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Nsemulwa aliiba mali ya Angel Helman mkazi wa kichangani.
Mtei ameongeza kuwa alifanikiwa kuiba Godoro,shuka pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki moja na elfu sitini vyote vikiwa na jumla ya thamani ya  zaidi ya shilingi laki tatu.
Kwa upande wake mshtakiwa amekana shitaka hilo  na mahakama imeahirisha shtaka hilo mpaka litakapotajwa tena tarehe 31 mei mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa tena na mshtakiwa yupo nje kwa dhamana.
Mwandishi:Rogate Tweve
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA