PEMBEJEO ZA RUZUKU MSIMU WA KILIMO 2015/2016 ILIKUWA CHANGAMOTO TUPU KWA WAKULIMA MANISPAA YA MPANDA


WAKATI msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017 ukitarajia kuanza mwezi Septemba mwaka huu,ripoti ya matumizi ya pembejeo Katika msimu uliopita wa 2015/2016 katika Manispaa ya Mpanda imeonesha kuwa ilitumia jumla ya pembejeo 27813 kati ya 32145 zilizoletwa katika Manispaa hiyo zimetumika.

Tarifa ya Kaimu Afisa kilimo Manispaa ya Mpanda Bw. Said Hemed iliyotolewa na Afisa habari wa Manispaa ya Mpanda Bw.Donald Pius ilionesha kuwa matumizi ya pembejeo katika msimu wa kilimo uliopita hayakutumika ipasavyo na kwa wakati kwa madai kuwa wizara ya kilimo kuchelewesha pembejeo hizo.
Baadhi ya wakulima Katika Manispaa ya Mpanda Bernard Nkana na Kapata Joseph walisema kuwa wamekuwa wakipata hasara kubwa ya sekta ya kilimo kutokana na pembejeo za kilimo kucheleweshwa.
Aidha walisema mbali na kucheleweshwa kwa mbolea na mbegu bado bei ya pembejeo hizo ni  kubwa  ukilinganisha na uwezo wa mkulima ambapo wametolea mfano kuwa  bei ya mbolea CAN na UREA ni shilingi 58,000/=.
Hata hivyo mawakala wasambazaji wa pembejeo za ruzuku wanalalamikiwa na wakulima kwa kutosambaza pembejeo hizo kwa wakati suala ambalo miongoni mwa mawakala waliozungumza na mtandao huu walisema kuwa tatizo la kuchelewa kwa pembejeo za kilimo siyo lao bali ni la serikali kuchelewa kuwakabidhi mbolea hizo.
Akitolea ufafanuzi wa mbegu na mbolea kuwa na bei ya juu,Afisa habari wa Manispaa Bw.Donald Pius kwa niaba ya Kaimu afisa kilimo Manispaa ya Mpanda alisema kuwa ndiyo bei elekezi ya serikali ambapo hata hivyo walisema kuwa wataishauri serikali kuleta mbolea mapema sanjari na kupitia upya gharama za pembejeo za kilimo.
Katika takwimu ya vocha za ruzuku zilizopokelewa na Manispaa zinaonesha kuwa mbolea ya kupandia zilikuwa 10,644,Mbolea ya kukuzia zilikuwa 10,644,mbegu za mahindi chotara 10,644 na mbegu za Mpunga 213 huku mbolea zilizotumika zinaonesha kuwa mbolea ya kupandia zilikuwa 9200, Mbolea ya kukuzia zilikuwa 9200, mbegu za mahindi chotara 9200 na mbegu za Mpunga 213
Miongoni mwa mazao yanayolimwa Mkoani Katavi kwa wingi ni pamoja na Mahindi,mihogo,mpunga,ulezi,ufuta  na karanga.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA