WATU 5 WAKIWEMO WATATU WENYE KADI 19 ZA ATM ZA BENKI WANASWA NA JESHI LA POLISI KATAVI



WATU watatu wakazi wa tarafa ya kashaulili wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na kadi za ATM 19 za watu tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Damas Nyanda amethibitisha Kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao pia wamekutwa za Kadi hizo na fedha Taslimu Kiasi cha Shilingi milioni 3,680,000.
Katika hatua nyingine Kamanda Nyanda amesema jeshi la polisi limewakamata watu wawili wakazi wa Mji wa Zamani kwa Kosa la Kukutwa na Nyara za Serikali pamoja na Bang vikiwa vimehifadhiwa kwenye kopo.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linatoa wito kwa wananchi Kutoa taarifa za uhalifu ili Wachukuliwe sheria.
Hata hivyo watuhumiwa majina yao hayajatajwa kwa sababu za kiuchunguzi zaidi.
Mwandishi : Issack Gerald Bathromeo
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA