WALIMU MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVIWAMEIOMBA SERIKALI KUWAPANDISHA VYEO WANAPOKUWA WAMEKIDHI VIGEZO.



WALIMU wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali kuwapandisha cheo wanapokuwa wamekidhi vigezo pamoja na kutengenezewa vitambulisho vipya  vya kazi.

Wamesema hayo jana katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Malando Manispaa ya Mpanda  kilichokuwa  na lengo la  kujadili changamoto za walimu.
Aidha wameongeza kuwa kutopandishwa cheo ni sehemu ambayo inamnyima haki mfanyakazi wakati ni haki yake.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni  amesema ili mfanyakazi yeyote apandishwe cheo ni lazima aonyeshe bidii ya kufanya kazi.
Wakati huo huo Kanoni ametumia nafasi hiyo kuwataka watumishi hewa katika manispaa ya Mpanda kurejesha fedha zote ambazo wamelipwa na serikali kipindi wakiwa kazini.
Mwandishi : Vumilia Abel
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA