WANNE MBARONI KATAVI KWA KUMILIKI SILAHA SMG,MWENZAO AFA KWA RISASI KATIKA MAJIBIZANO NA POLISI.


Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu wanne wakazi wa kata ya Mishamo Wilayani Mpanda wakituhumiwa kumiliki silaha kinyume na sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake,kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi SSP Damas Nyanda amesema,watuhumiwa hao walikamatwa Mnamo Aprili 22 mwaka huu katika kijiji cha cha Bosongola Kata ya Mishamo wakiwa na silaha aina ya SMG yenye namba za usajili TX5971-1996 ikiwa  na magazine mbili zenye jumla ya  risasi 86 ambapo magazine ya kwanza ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi 31 huku magazine kubwa ikiwa  na uwezo wa kubeba risasi 45.
Katika ukamataji huo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata nyama ya kiboko kilo mbili iliyokuwa inapikwa kwenye sufuria jikoni.
SSP Nyanda amewataja watuhumiwa kuwa ni James Amos Samandale (28),Amos Maliyatabu Samandale (70),Leoben Kagoma Karumanzira(25) na Kulwa Joseph Daniel wote wakazi wa Mishamo.
Aidha Kamanda nyanda amesema wakati msako ukiendelea kufanyika jeshi la polisi walikutana na watuhumiwa watatu wakiwemo Harumkiza (28),Kulwa Joseph Daniel na mwenzao ambaye bado anatafutwa ambapo watuhumiwa hao walikataa amri ya askari iliwataka kusimama na badala yake kukazuka majibizano baina ya askari polisi na watuhumiwa hao na hatimaye Harumkiza Joshua akapigwa risasi na kufa papo hapo.
Mwili wa marehemu uliokuwa umelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya uchunguzi kufanyika.
Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika
Halikadhalika katika majibizano hayo ya risasi,pikipiki moja yenye namba za usajili T241CKZ SANLG pamoj na kitambulisho cha kupigia kura vilivyobainika kuwa mali ya mtuhumiwa aliyetoroka vilikamatwa.
Hata hivyo Kamanda amewaonya wananchi wanaomiliki silaha kinyume na sheria ambapo pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uharifu ili udhibitiwe kabla ya kusababisha madhara kwa jamii.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA